Benki ya Dunia na Ethiopia zasaini makubaliano ya kufufua maeneo yaliyoathiriwa na migogoro
2022-05-17 09:04:14| cri


 

Serikali ya Ethiopia na Benki ya Dunia jana zimesaini makubaliano ya ufadhili wa dola za kimarekani milioni 300 ili kusaidia ukarabati wa maeneo yaliyoathiriwa na migogoro nchini humo.

Makubaliano hayo yalisainiwa na waziri wa fedha wa Ethiopia Bw. Ahmed Shide na mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Ethiopia Bw. Ousmane Dione.

Kutokana na taarifa iliyotolewa jana na wizara ya fedha ya Ethiopia, fedha hizo zitatumika kusaidia jamii katika maeneo yaliyoathiriwa na migogoro kupata tena huduma za kimsingi za elimu, afya na usambazaji wa maji.