Mali yatangaza kujiondoa kutoka G5 Sahel
2022-05-17 09:06:31| cri

Serikali ya mpito ya Mali imetangaza kuwa itajiondoa katika taasisi zote za kundi la G5 Sahel, likiwemo jeshi lake la pamoja la kupambana na ugaidi.

Katika taarifa yake iliyotolewa jumapili, Serikali ya mpito ya Mali imesema mkutano wa kilele wa kundi hilo ulipangwa kufanyika mjini Bamako, Mali, mwezi Februari mwaka huu, ambapo Mali ilipaswa kuwa rais wa zamu, lakini mkutano huo bado haujafanyika.

Taarifa hiyo imesema Mali inaamini kuwa jambo hilo ni ukiukaji wa maamuzi ya awali na kanuni zake za kimsingi, na kuchukua hatua ya kujiondoa katika Kundi hilo.