Wagombea urais nchini Kenya watangaza majina ya wagombea wenza
2022-05-17 09:06:42| CRI

Wagombea wawili wa nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Agosti 9 nchini Kenya wamewataja wagombea wenza.

Jumapili iliyopita, Naibu rais wa Kenya William Ruto anayewania nafasi ya urais chini ya muungano wa Kenya Kwanza, alikuwa wa kwanza kumtaja mgombea mwenza wake, Rigathi Gachagua, mbunge kutoka kaunti ya Nyeri katikati ya Kenya, baada ya kikao cha saa 17 kati ya Ruti na washirika kufikia uamuzi huo.

Mara baada ya Ruto kumtambulisha mgombea mwenza wake, Raila Odinga, waziri mkuu wa zamani wa Kenya, jana alimtangaza Martha Karua kuwa mgombea mwenza. Hatua hiyo inatarajiwa kuwashawishi wapiga kura wanawake huku ikiongeza mvutano katika mbio za nafasi ya urais nchini humo.