Angola inakisiwa kuwa na hifadhi ya mapipa bilioni 4 ya mafuta
2022-05-18 08:48:22| CRI

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mafuta, Gesi na Gesi Asilia nchini Angola Paulino Jeronimo amesema, hifadhi ya mafuta nchini humo inakadiriwa kufikia mapipa bilioni nne.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 8 wa Nchi zinazozalisha Mafuta Afrika (CAPE VIII) uliofanyika nchini humo, Jeronimo amesema wingi huo unamaanisha kuna mengi ya kuendelezwa ili kuweza kutuliza uzalishaji wa mafuta ghafi nchini humo, na kwamba changamoto kubwa ni kuboresha na kuimarisha mbadala wa hifadhi hiyo kwa lengo la kupunguza kushuka kwa kasi kwa uzalishaji.

Amesema uzalishaji wa mafuta nchini Angola ulifikia kilele chake mwaka 2008, wakati ilipozalisha mapipa milioni 1.9 ya mafuta kwa siku, huku uzalishaji wa sasa ukikadiriwa kufikia mapipa milioni 1.2 kwa siku.