Tanzania yapanga kumwagilia hekta milioni 1.2 za mashamba hadi kufikia mwaka 2025
2022-05-18 08:52:00| CRI

Waziri wa Kilimo wa Tanzania Hussein Bashe amesema nchi hiyo inapanga kumwagilia hekta milioni 1.2 za mashamba hadi kufikia mwaka 2025.

Bashe amesema serikali kupitia Tume ya Umwagiliaji inatekeleza mpango kabambe unaolenga kuboresha kilimo cha umwagiliaji, na kuongeza kuwa eneo la kilimo cha umwagiliaji litaongezeka kutoka hekta 727,280.6 mwaka 2021/2022 hadi hekta 822,285.6 mwaka 2022/2023.

Bashe amezindua mpango wa kupanua kilimo cha umwagiliaji wakati alipowasilisha makadirio ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2022/2023 unaoanza Julai Mosi, 2022 hadi Juni 30, 2023.

Ameliambia Bunge kuwa Tume hiyo pia itajenga mabwawa 14 kwa ajili ya kupata maji mita 131,535,000 za ujazo kwa ajili ya umwagiliaji.