Benki ya Maendeleo ya Afrika yazitaka nchi za Afrika zikuze miji yenye ukubwa wa kati
2022-05-19 08:45:28| cri


 

Ofisa mwandamizi wa maendeleo ya miji katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Babati Mokgethi jana amesema, nchi za Afrika zinapaswa kuboresha huduma muhimu kama makazi, elimu, maji safi na afya katika miji yenye ukubwa wa kati, ili kuiwezesha kuwa vizuizi dhidi ya uhamiaji usiodhibitiwa wa kutoka vijijini kwenda mijini.

Mokgethi amesema suluhisho la mlipuko wa idadi ya watu, uhalifu, umaskini na uchafuzi wa mazingira katika miji mikubwa barani Afrika ni kuboresha miji yenye ukubwa wa kati.

Pia ameongeza kuwa ni muhimu kuelekeza kundi kubwa la wakazi wa mashambani barani Afrika kwenye miji yenye ukubwa wa kati ili kupunguza shinikizo kwa miji mikubwa.