Idadi ya vifo katika mlipuko wa gesi nchini Nigeria yafikia 9
2022-05-19 08:34:23| cri

Mratibu wa Shirika la Usimamizi wa Masuala ya Dharura (NEMA) katika mkoa wa Kano, kaskazini magharibi mwa Nigeria, Bw. Nuradeen Abdullahi amethibitisha kuwa, watu tisa wamefariki na wengine 10 kujeruhiwa baada ya mtungi wa gesi kulipuka Jumanne jioni katika mkoa huo.

Bw. Abdullahi ametoa wito kwa umma, hasa wale wanaoishi katika eneo lililoathiriwa, kuwa watulivu na kuonya dhidi ya kueneza habari zisizo za kweli kuhusu ajali hiyo.