TPA yafungua ofisi katika nchi jirani zisizo na bandari
2022-05-20 08:37:25| CRI

Mamlaka ya Bandari nchini Tanzania (TPA) imefungua ofisi za mawakala katika nchi jirani zisizo na bandari ili kuvutia biashara zaidi.

Hayo yamesemwa jana na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Dodoma. Amesema ofisi hizo zimefunguliwa katika nchi za Rwanda, Malawi, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), na zimepewa kazi ya kuvutia wafanyabiashara watumie bandari za Tanzania.

Amesema hatua hiyo imekuja kufuatia kuongezwa ubora wa bandari za Dar es Salaam, Mtwara, na Tanga.