Rais wa Msumbiji asema ugaidi katika nchi hauchochewi na mizozo ya kidini
2022-05-20 08:32:57| cri

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi amesema vitendo vya kigaidi mkoani Cabo Delgado, kaskazini mwa nchi hiyo si matokeo ya mizozo ya kidini.

Rais Nyusi amesema hayo mjini Maputo alipozungumza na wamishionari wa kigeni walioko ziarani nchini humo. Amesema watu wengi wanahusisha ugaidi katika mkoa huo kuwa ni matokeo ya migogoro ya kidini, jambo lisilo la kweli, kwani kati ya magaidi hao kuna watu wa aina zote, wa dini tofauti, uraia tofauti, na rangi tofauti.

Ameongeza kuwa, Msumbiji si taifa lisiloongozwa na dini moja, na anachukulia dini kama sehemu ya suluhisho la maendeleo.