Maonyesho ya sanaa za kisasa za Afrika yafunguliwa huko Dakar
2022-05-20 08:33:38| cri


 

     Maonyesho ya 14 ya sanaa za kisasa za Afrika yanayofanyika kila baada ya miaka miwili yamefunguliwa jana huko Dakar nchini Senegal, na China imeshiriki kwenye maonyesho hayo kama mgeni mwalikwa kwa mara ya kwanza.

     Rais wa Senegal Macky Sall alishiriki hafla ya ufunguzi wa maonyesho hayo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Michezo wa Kitaifa wa Senegal uliojengwa kwa msaada wa China, na kazi za sanaa kutoka nchi 28 duniani zitaonyeshwa.

     Balozi wa China nchini Senegal Xiao Han amesema, hii ni mara ya kwanza kwa maonyesho hayo kutoa mwaliko kwa nchi nje ya Afrika kama mgeni mkuu. Amesema China itaonesha sanaa zake za kisasa na ubunifu wa wasanii wa China kwa watazamaji wa Afrika, jambo litakalozidisha maelewano na urafiki kati ya wananchi wa pande hizo mbili.