Watu wenye silaha waua watu 360 katika miezi mitatu iliyopita kusini magharibi mwa Nigeria
2022-05-20 08:34:32| CRI

Watu 360 wameuawa na wengine 1,389 kutekwa nyara katika robo ya kwanza ya mwaka 2022, katika mashambulizi yaliyofanywa na watu wenye silaha katika Jimbo la Kaduna, kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Kwa mujibu wa ripoti ya usalama iliyotolewa jana Alhamisi, serikali ya Jimbo la Kaduna imesema watu 258 walijeruhiwa katika mashambulizi mbalimbali na kesi 10 za ubakaji zilizorekodiwa kati ya mwezi Januari hadi Machi. 

Serikali hiyo imethibitisha uwepo wa makundi yenye itikali kali likiwemo kundi la Boko Haram, kwenye baadhi ya sehemu za jimbo hilo, na kwamba kuna dalili kuwa wapiganaji wa kundi lenye itikadi kali waliohama kutoka eneo la kaskazini mashariki wana uhusiano mkubwa na makundi ya wahalifu yenye silaha kwenye jimbo hilo.