UNHCR yasema Ethiopia inaendelea kukabiliwa na idadi kubwa ya watu wanaokimbia makazi yao
2022-05-20 08:36:32| CRI

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limesema, Ethiopia inaendelea kukabiliwa na hali sugu ya watu kukimbia makazi yao kutokana na mapigano, vurugu kati ya makabila tofauti, majanga ya kimaumbile na athari za mabadiliko ya tabianchi, hususan katika mikoa ya Oromia, Benishangul Gumuz na Somali.

Takwimu zilizotolewa na UNHCR zimeonyesha kuwa, mpaka kufikia mwezi Machi, inakadiriwa kuwa watu 5,582,000 walikimbia makazi yao nchini humo kutokana na mapigano ya kutumia silaha na majanga ya asili.

Shirika hilo limesema, licha ya changamoto zinazoendelea za kiusalama, limefanikiwa kuchukua nafasi muhimu, ikiwemo kuongoza mchakato wa kuwarejesha wakimbizi wa ndani katika mikoa ya Tigray, Afar, Amhara na Somali.