Mapambano makali kati ya jeshi la DRC na Kundi la M23 yaanza tena
2022-05-23 14:31:29| CRI

Msemaji wa FARDC Kanali Ndjike Kaiko amesema mapambano makali kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Kundi la waasi lijulikanalo kama “The March 23 Movement” (M23) yameanza tena mapema jana huko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Kanali Kaiko amesema FARC ilianza kufanya mashambulizi dhidi ya Kundi la M23 kuanzia Jumapili asubuhi katika eneo la Rutshuru mkoani Kivu Kaskazini, ambapo Jeshi la DRC linaendelea kuongoza dhidi ya maadui wao. Jeshi la taifa linataka kumaliza unafiki wa waasi wa M23 kwa njia timilifu, kwasababu waasi hao hawataki kutimiza amani kwa dhati. Kutokana na kurejeshwa kwa operesheni hizi, jeshi la taifa litadhibiti tena vilima vinavyotumiwa na waasi kama kituo chao, na kuwaletea tena wananchi amani.