Baraza la Afya Duniani kufuatilia COVID-19, Afya na amani
2022-05-23 09:00:40| CRI

Mkutano wa 73 wa Baraza la Afya Duniani (WHA) umeanza jana huko Geneva, Uswiss, ambapo utafuatilia masuala makubwa yakiwemo janga la COVID-19 na afya ya dunia inavyohimiza pendekezo la amani.

Janga la COVID-19 linaendelea kuwa moja ya vipaumbele vya mkutano wa mwaka huu wa WHA ambao ni wa kwanza kufanyika ana kwa ana tangu janga hilo litokee zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dr. Tedros Ghebreyesus amesisitiza kuwa janga la COVID-19 bado halijatokomezwa. Ametoa mwito kwa nchi zote kutimiza lengo la kuchanja asilimia 70 ya watu haraka iwezekanavyo.