Rwanda yataka ufanyike uchunguzi juu ya makombora ya DRC yaliyowajeruhi raia
2022-05-24 09:18:19| CRI

Jeshi la Rwanda (RDF) limesema kuwa makombora yaliyorushwa na kikosi cha wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC) katika eneo lake la mashariki yalishambulia kaskazini mwa Rwanda na kusababisha raia kadhaa kujeruhiwa na kuharibu mali.

Roketi hizo zilipiga maeneo ya Kinigi na Nyange katika wilaya ya Musanze iliyoko mpakani mwaa nchi hizo mbili.

Msemaji wa jeshi la Rwanda Kanali Ronald Rwivanga amesema kuwa waliojeruhiwa wamepatiwa matibabu na maafisa wanatathmini kiwango cha uharibifu.

RDF imeomba ufanywe uchunguzi wa haraka na Mfumo wa Uthibitishaji wa Pamoja wa Kikanda, ambao ni wa kijeshi kwa nchi kadhaa za eneo la Maziwa Makuu.

Aidha Mamlaka ya Rwanda pia inawasiliana na wenzao wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuhusu tukio hilo, na sasa hali katika eneo hilo imerejea na kuwa ya kawaida na usalama umehakikishiwa.