Kenya na Uganda kufanya uuzaji wa pamoja ili kuvutia watalii wa nje
2022-05-24 09:24:56| CRI

Kenya na Uganda zinatarajiwa kuanza kufanya shughuli za uuzaji wa pamoja ili kuvutia watalii kutoka nje.

Akiongea kwenye uzinduzi wa maonesho ya barabarani yaliyoandaliwa na Bodi ya Utalii ya Uganda (UTB), Mkurugenzi Mkuu wa Shirikisho la Waendesha Utalii wa Kenya Fred Kaigua amesema jijini Nairobi kuwa ushirikiano wa wadau wa utalii wa Kenya na Uganda utasaidia sekta hiyo kuondokana na athari za janga la UVIKO-19. Amesema sekta hii ina uhusiano wa karibu kwasababu wana vivutio vya aina mbalimbali ambavyo vitahimiza wageni kufika kwenye kanda hiyo.

Naye meneja mauzo wa UTB, Clare Mugabi amesema ukuaji wa sekta ya utalii nchini Kenya pia utaleta athari chanya kwenye sekta ya usafiri ya Uganda, kwani watalii wa kigeni watakaokwenda Kenya na baadaye kwenda Uganda watapata uzoefu mzuri wa usafiri kupitia urithi ulioshiba wa utamaduni wa Afrika.