Benki ya AfDB yafanya mikutano ya mwaka nchini Ghana
2022-05-25 10:36:09| CRI

Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB imefungua mikutano yake ya mwaka 2022 huko Accra, Ghana ikihudhuriwa na viongozi, wanasiasa na wanateknolojia wa Afrika.

Rais Nana Addo Dankwa wa Ghana kwenye ufunguzi wa mikutano hiyo amewataka wakopeshaji wa masharti nafuu wa bara hilo kuisaidia Afrika kukusanya rasilimali za fedha zinazohitajika sana katika mabadiliko yake.

Rais huyo amesema, athari mbalimbali zinazotokana na maambukizi ya COVID-19 na mgogoro wa nishati uliopo sasa duniani unaosababishwa na mapambano kati ya Russia na Ukraine zimeleta mzigo mkubwa wa madeni kwa nchi za Afrika.

Pia ameitaka AfDB kuongeza mchango wake katika upatikanaji wa rasilimali za fedha ili kuhimiza maendeleo ya bara la Afrika.