Ofisa wa UM asema mapambano kati ya Ukraine na Russia yanaharibu utendaji wa uchumi wa Afrika
2022-05-25 10:37:02| CRI

Mjumbe wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP nchini Kenya Bw. Walid Badawi amesema, mapambano kati ya Ukraine na Russia yanaathiri vibaya utendaji wa uchumi wa Afrika.

Bw. Badawi amesema, mgogoro huo umesababisha ongezeko kubwa la gharama ya bidhaa za msingi barani humo.

Akiongea kwenye mkutano kando ya kongamano la ngazi ya juu kuhusu kuhamasisha uwekezaji wa malengo ya maendeleo endelevu ya Afrika, amesema kuwa nchi nyingi za Afrika zinanunua nafaka kutoka nje, na zinategemea kwa kiasi kikubwa mauzo ya ngano ya Russia na Ukraine. Sasa mnyororo huu wa thamani umeathiriwa na unaweza kuzidisha hali mbaya ya usalama wa chakula.

Ameongeza kuwa tangu mapambano kati ya Ukraine na Russia yatokee mwezi Februari, bei ya mafuta katika soko la kimataifa imeongezeka na kusababisha gharama kubwa ya matumizi ya nishati barani Afrika.