Tanzania kununua ndege tano ili kuhimiza maendeleo ya sekta ya usafiri wa anga nchini
2022-05-25 10:32:21| CRI

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Tanzania Bw. Makame Mbarawa alisema Tanzania inapanga kutumia shilingi bilioni 468 (sawa na dola takriban milioni 201 za kimarekani) kwa ajili ya kununua ndege tano mpya ili kuhimiza maendeleo ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL).

Mbarawa amesema katika mwaka ya fedha wa 2022/2023 utakaoanzia Julai mosi mwaka 2022 hadi Juni 30 mwaka 2023, serikali ya Tanzania inapanga kununua ndege tano, ikiwa ni pamoja na Boeing moja ya 787-8 Dreamliner, Boeing mbili za 737-9, ndege moja ya mzigo ya Boeing 767-300F na moja ya Dash-8 Q400. Serikali imeshasaini makubaliano ya ununuzi wa ndege hizo tano.

Ameongeza kuwa serikali inadhamiria kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha usafiri na uchukuzi katika eneo la Afrika Mashariki na Kati.