Reli ya SGR ya Kenya yaongeza kasi ya usafirishaji wa mizigo mingi na kuchochea ukuaji
2022-05-26 10:53:28| CRI

Huduma ya Mizigo ya Reli ya SGR kati ya Mombasa na Nairobi imetoa urahisi wa usafirishaji wa mizigo mingi inayokwenda katika nchi zisizo na bahari tangu kuzinduliwa kwake Januari 2018.

Edward Opiyo, Meneja kituo katika Vituo vya reli ya Mizigo mjini Nairobi ambayo ni kampuni binafsi inayohusiana moja kwa moja na huduma za mizigo za SGR, amesema imetoa njia ya kasi, ufanisi na ya gharama nafuu katika kusafirisha mizigo mingi.

Katika mahojiano ya hivi karibuni na Shirika la Habari la China Xinhua kuelekea maadhimisho ya miaka mitano ya uzinduzi wa reli hiyo ya kisasa, Opiyo amesema huduma hizo zimepandisha hadhi ya Kenya kama msafirishaji na kitovu cha usambazaji.