Mapato ya chai ya Kenya yaongezeka kwa asilimia 10 katika robo ya kwanza ya mwaka huu
2022-05-26 10:56:46| CRI

Bodi ya Chai ya Kenya jana ilitangaza kuwa ingawa mapambano kati ya Russia na Ukraine yameathiri shughuli za uchukuzi, lakini mapato ya chai ya Kenya inayouzwa nje yameongezeka kwa asilimia 10.4 katika robo ya kwanza ya mwaka 2022 ikilinganishwa na mwaka jana kutokana na ongezeko la bei duniani.

Kenya imeingiza shilingi bilioni 39.5 sawa na dola milioni 339 za kimarekani ndani ya miezi miatu baada ya kuuza nje tani 135,721 za chai, kiasi ambacho kimeongezeka kutokana na ongezeko la bei ikilinganishwa na dola milioni 307 za kimarekani baada ya kuuza nje tani 152,633 za chai katika robo ya kwanza ya mwaka jana.

Katika robo ya kwanza ya mwaka huu bei ya wastani ya chai duniani imekuwa dola 3 za kimarekani kwa kilo, kiasi ambacho kimeongezeka kikilinganishwa na cha mwaka jana wakati kama huu ambacho ni dola 2.7 za kimarekani.