Tanzania yaanza msako wa kilimo cha bangi
2022-05-26 10:52:19| CRI

Mamlaka za kupambana na dawa za kulevya Tanzania zimeanza msako wa nchi nzima kwa watu wanaolima bangi.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya (DCEA) Gerald Kusaya amesema Jumatano kuwa heka 21 za bangi zilizogunduliwa katika wilaya za Arumeru na Monduli mkoani Arusha zimeharibiwa tangu msako uanze Mei 20, na kuongeza kuwa msako umeanza mkoani humo kwa sababu mkoa huo unasifika vibaya kwa ulimaji wa bangi. Aidha amebainisha kuwa washukiwa wawili wamekamatwa wakihusishwa na umiliki wa mashamba ya bangi, na wengine wawili wamepatikana wakibeba kilo 220 za bangi kwenye pikipiki.

Amefafanua kuwa msako huo uliofanywa na DCEA ikishirikiana na vyombo vya usalama wakiwemo polisi, utaendelea na utafanyika katika mikoa yote nchini.