Huawei yaimarisha mafunzo ili kupanua kundi la watu wenye ujuzi wa TEHAMA nchini Kenya
2022-05-26 10:58:26| CRI

Ofisa mkuu wa mahusiano ya umma wa tawi la kampuni ya Huawei ya China nchini Kenya Bw. Dalmar Abdi amesema, nchi hiyo imeimarisha utoaji wa mafunzo, ili kupanua kundi la watu wenye ujuzi wa TEHAMA nchini Kenya.

Bw. Abdi amesema hayo wakati akitembelea kituo cha mafunzo cha Huawei, na kueleza kuwa kampuni hiyo inafanya juhudi kuziba pengo la utoaji wa mafunzo na vyeti vya TEHAMA nchini Kenya.

Ameongeza kuwa ili kutimiza lengo hilo, kampuni ya Huawei imeshirikiana na taasisi 80 za elimu ya juu kutoa mafunzo ya ujuzi wa TEHAMA kwa wanafunzi kupitia mashine za kisasa.

Kituo cha mafunzo ya Huawei kiko katika Taasisi ya Mawasiliano ya Ngazi ya Juu ya Afrika AFRALTI huko Nairobi, ambacho kinatarajia kuandaa wataalamu 200 wa ngazi ya juu wa TEHAMA na watu 5000 wenye ujuzi na uzoefu wa TEHAMA. Mbali na hayo, kampuni hiyo inapanga kutoa mafunzo kwa watumishi 2,500 wa umma na wahitimu, wanafunzi na vijana 12,000 nchini Kenya.