Benki kuu ya Kenya yafungua jengo lililojengwa na kampuni ya China
2022-05-27 09:18:25| CRI

Benki kuu ya Kenya CBK imefungua jengo lililojengwa na kampuni ya China (CBK Pension Towers), ambalo liko katika kitovu cha Nairobi, nchini Kenya.

Kampuni ya ujenzi ya Wu Yi ya China imejenga jengo hilo la kisasa ambalo lina majengo marefu pacha yenye urefu wa mita 110. Jengo hilo lina sehemu mbili zinazounganishwa za ofisi, na iliyo refu zaidi ina ghorofa 27 na nyingine ina ghorofa 24.

Wakati akizindua rasmi jengo hilo, rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema, kufuatia kufunguliwa kwa jengo hilo refu jijini Nairobi, Kenya imepata jengo jingine jipya la kipekee na lililotumia usanifu wa kisasa.

Rais huyo pia amesema, jengo hilo limetumia teknolojia ya kijani kwa kuwekwa taa zinazotumia nishati ya jua.