Sudan yaondoa hali ya dharura ya nchi nzima
2022-05-30 10:04:58| CRI

Mwenyekiti wa baraza la mamlaka ya mpito la Sudan Jenerali Abdel Fattah Al-Burhan, ametoa amri ya kuondoa hali ya dharura katika maeneo yote ya Sudan.

Taarifa iliyotolewa na baraza hilo inasema hatua hiyo imechukuliwa ili “kuandaa mazingira ya mazungumzo yenye nia njema yatakayoleta utulivu katika kipindi cha mpito”.

Sudan imekuwa ikikumbwa na msukosuko wa kisiasa baada ya Bw. Al- Burhan ambaye pia ni mkuu wa majeshi wa Sudan, kutangaza hali ya dharura kuanza Oktoba 25 mwaka jana, na kuvunja baraza lenye mamlaka na serikali ya nchi hiyo.

Kuanzia wakati huo mji wa Khartoum na miji mingine imekumbwa na maandamano ya mara kwa mara yakihitaji kurudishwa kwa utawala wa kiraia.