Watu 37 wauawa kutokana na shambulizi nchini DRC lililofanywa na Kundi la ADF
2022-05-30 10:01:08| CRI

Kundi la waasi la ADF la Uganda terehe 28 lilifanya shambulizi kwenye kijiji cha Beu-Manyama kilichoko eneo la Beni mkoani Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), na kusababisha idadi ya vifo vya watu kuongezeka kutoka 21 hadi 37.

Miili 16 mipya iligunduliwa tarehe 29 katika eneo karibu na kijiji cha Beu-Manyama. Habari kutoka jamii ya huko zinasema watu hao walikuwa mateka waliotekwa na waasi tarehe 28.

Katika tarehe 28 kundi la ADF liliwaua raia 21 na kuteketeza nyumba 8 katika kijiji cha Beu-Manyama. Jeshi la DRC limesema kwenye mapambano dhidi ya kundi la ADF, waasi saba wameuawa na mwingine mmoja amekamatwa.