Washirika wa misaada ya kibinadamu waonya kutokea kwa njaa kali Afrika Mashariki kutokana na uhaba wa mvua
2022-05-31 09:03:53| CRI

Muungano wa mashirika ya hali ya hewa na washirika wa misaada ya kibinadamu umeonya kwamba litakuwepo tishio kubwa la njaa kali katika Afrika Mashariki baada ya mvua kutonyesha kwa misimu minne.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa Jumatatu, na mashirika 12 yakiwemo FAO, UNHCR, UNOCHA, WFP, UNICEF na IGAD imeonya kwamba hali inaweza kuwa mbaya zaidi kutokana na utabiri unaoonesha kuwa msimu wa tano unaoanzia Oktoba hadi Disemba pia utakosa mvua. Taarifa hiyo imeongeza kuwa ukame mkali uliopo sasa, unaosambaa na unaoendelea kudumu ambao umeathiri Somalia, maeneo kame na nusu kame ya Kenya, na maeneo ya ufugaji ya mashariki na kusini mwa Ethiopia, si wa kawaida.