Ethiopia kupokea msaada wa dola milioni 200 kutoka Benki ya Dunia
2022-06-02 09:53:49| CRI

Ethiopia inatazamiwa kupokea msaada wa dola milioni 200 za Kimarekani kutoka Benki ya Dunia.

Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Ustadi wa Ethiopia Muferiat Kamil jana alisema kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook kuwa fedha hizo zitatumika kuandaa wafanyakazi wenye ujuzi na kuongeza uwezo wa taasisi za mafunzo ya kiufundi za kiserikali.

Kamil alisema alifanya mazungumzo na maafisa wa Benki ya Dunia kuhusu njia za kutoa nafasi za ajira za hali ya juu kwa Waethiopia. Pande zote mbili pia zilifanya majadiliano ya kupanua mawazo ya kimkakati.

Serikali ya Ethiopia na Benki ya Dunia mwezi Mei zilitia saini makubaliano ya ufadhili wa dola za kimarekani milioni 300 kusaidia ukarabati na ufufuaji wa maeneo yaliyoathiriwa na migogoro ya Ethiopia. Fedha hizo zitatumika kusaidia jamii katika maeneo hayo kupata huduma za msingi za elimu, afya na usambazaji wa maji.