UNHCR lasema Waafrika 132 wanaotafuta hifadhi wahamishwa kutoka Libya hadi Rwanda
2022-06-02 09:55:51| CRI

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) lilisema kwamba limewahamisha watu 132 wanaotafuta hifadhi wakiwemo watoto wadogo na wachanga, kutoka Libya hadi mahali salama nchini Rwanda.

Wakimbizi hao wanaotoka nchi tofauti za Afrika, wamekuwa wakiishi katika maeneo ya mji wa Tripoli, wakiwemo manusura wa ghasia na mateso na wanawake na wasichana walio hatarini.

Kaimu Mkuu wa UNHCR anayeshughulikia wakimbizi nchini Libya Bw. Djamal Zamoum amezitaka nchi nyingine kutoa njia zaidi au fursa za makazi mapya ili kuwasaidia na wengine kupata usalama nje ya Libya.