UM waonya kuwepo kwa hali mbaya na ya kutisha nchini Somalia kufuatia ukame mkali
2022-06-02 09:49:25| CRI

Shirika la misaada ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa limeonya kuwa mamilioni ya Wasomali walioathirika na ukame watakuwa na hali mbaya zaidi kutokana na kuongezeka kwa baa la njaa.

Kwenye taarifa yake aliyoitoa Jumanne jioni huko Mogadishu, Adam Abdelmoula, Mratibu Mkazi wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, ametoa wito kwa washirika wa maendeleo kuchukua hatua haraka na kusaidia kuongeza rasilimali zinazoendana na mahitaji yanayokua kwa kasi, pamoja na kuokoa maisha ya watu wengi zaidi nchini Somalia. Amesema kutokana na rasilimali chache zilizopo, kuanzia Januari hadi Aprili wameweza kuwafikia watu milioni 2.4 kati ya wale wote wenye mahitaji ya kibinadamu.

Abdelmoula amesisitiza kuwa hali ni mbaya sana na ya kutisha, kwani watu milioni 7.1 wataathirika na ukame kabla ya mwishoni mwa mwaka huu.