Huawei yaongeza kuajiri wataalamu wa Tehama wa Kenya kufuatia biashara yake kukua
2022-06-02 09:48:45| CRI

Kampuni ya mawasiliano ya simu ya China Huawei imesema kuwa imeimarisha juhudi za kuchukua wataalamu zaidi wa TEHAMA nchini Kenya kwa kuanza mpango wake wa taifa wa kuajiri wataalamu, ambapo biashara yake ikiendelea kukua, wataalamu wengi wenyeji wenye vipaji wanahitajika zaidi.

Akiongea kwenye maonesho ya kuvutia ajira ya Huawei jijini Nairobi, Naibu Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Huawei katika Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya umma Fiona Pan amesema Huawei ina nafasi 35 za ajira na nafasi nyingine 15 kwa washirika wake, ambazo zitahusu wafanyakazi wa muda na wa kudumu.

Pan amebainisha kuwa Huawei imeazimia kutoa mafunzo ya teknolojia na kuajiri watu wenye vipaji vikubwa na ndio maana wameandaa maonesho hayo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ili kupata fursa zilizopo hasa kwa wale wanaotaka kujishughulisha na Tehama. Amesema sekta ya Tehama inaendelea kukua zaidi na mahitaji ya wataalamu wa teknolojia wenye sifa katika sekta zote za uzalishaji yatakuwa makubwa katika siku za mbele.