Watu wengi wauawa kwenye shambulizi dhidi ya kanisa nchini Nigeria
2022-06-06 09:40:30| cri


 

Watu wasiojulikana waliokuwa na silaha wamewaua waumini kadhaa katika shambulizi dhidi ya kanisa kwenye mji wa Owo, jimbo la Ondo kusini magharibi mwa Nigeria jana.

Ofisa wa serikali ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema, watu hao wenye silaha walilipua mabomu karibu na madhabahu ya kanisa kabla ya kuwafyatulia risasi waumini, na kuwaua watu wengi.

Gavana wa jimbo la Ondo Bw. Arakunrin Akeredolu alithibitisha shambulizi hilo, lakini hakutoa maelezo zaidi kuhusu watu waliopoteza maisha ama washambuliaji.