Raia zaidi ya 38 wauawa katika shambulizi nchini DRC
2022-06-07 09:02:50| cri

Msemaji wa jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Bw. Jul Ngongo amethibitisha kuwa raia zaidi ya 38 wameuawa katika shambulizi lililofanywa na waasi wa kundi la Democratic Alliance la Uganda dhidi ya kijiji kimoja katika jimbo la Ituri kaskazini mashariki mwa nchi hiyo Jumapili usiku.

Bw. Ngongo amesema idadi kamili ya watu waliopoteza maisha katika shambulizi hilo bado haijulikani, na kwamba jeshi la serikali linawasaka watu wanaoshukiwa kuhusika na shambulizi hilo.