UNICEF yaomba fedha ili kuokoa maisha ya watoto Afrika Mashariki
2022-06-08 08:43:20| CRI

Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limeomba fedha za dharura ili kukwepa mlipuko wa vifo vya watoto unaoweza kutokea Afrika Mashariki kama jamii ya kimataifa haitachukua hatua za haraka.

Naibu Mkurugenzi wa UNICEF kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Rania Dagash amesema, zaidi ya watoto milioni 1.7 katika nchi za Ethiopia, Kenya na Somalia wanahitaji matibabu ya dharura ya utapiamlo mkali. Amesema nchi hizo zimerekodi idadi kubwa ya watoto wanaokabiliwa na utapiamlo mkali waliolazwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu katika robo ya kwanza ya mwaka huu ikilinganishwa na idadi hiyo kwa mwaka 2021.