Rais wa mpito wa Mali asaini amri ya kuongeza muda wa mpito wa kisiasa
2022-06-08 08:45:08| CRI

Rais wa mpito wa Mali Assimi Goita, jumatatu wiki hii amesaini amri ya kuongeza muda wa mpito wa kisiasa nchini Mali kwa miezi 24 kuanzia Machi 26 mwaka huu.

Uamuzi ho umekuja siku mbili baada ya Mkutano maalumu wa sita wa viongozi wa nchi na serikali za Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS)uliofanyika mjini Accra, Ghana. Viongozi hao walishindwa kufikia makubaliano juu ya kuondolewa kwa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Mali.

Pia waliamua kutathmini upya hali ya Mali Julai 3, huku wakipendekeza kuendelea na mazungumzo, ili kufikia makubaliano ya kuhakikisha “vikwazo vinaondolewa kwa utaratibu” kwani masharti ya mpito yamefikiwa.