Watu zaidi ya 22 wauawa katika shambulizi dhidi ya kanisa nchini Nigeria
2022-06-08 08:52:51| cri

Mkuu wa Idara ya usimamizi wa mambo ya dharura ya Nigeria katika jimbo la Ondo Bw. Kadiri Olanrewaju, amethibitisha kuwa watu zaidi ya 22 waliuawa na wengine 50 kujeruhiwa katika shambulizi dhidi ya kanisa katika jimbo la Ondo, kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Takriban watu 700 walikuwa wamekusanyika kanisani wakati wa shambulizi hilo, na huenda kuna majeruhi ambao bado hawajafahamika.