Naibu mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing ametoa wito wa kulinda amani na utulivu kwenye kanda ya Afrika ya kati
2022-06-09 08:44:15| CRI

Naibu mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing ametoa wito wa kulinda amani na utulivu kwenye kanda ya Afrika ya kati.

Balozi Dai Bing ametoa wito huo katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu usalama katika eneo la Afrika ya kati uliofanyika jana jumatano. Amesema, jumuiya ya kimataifa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa kanda ya Afrika ya kati inatakiwa kuunga mkono nchi za kanda hiyo kuimarisha utawala na ujenzi wa uwezo kwa kufuata hali ya nchi hizo, kutatua masuala ya nchi hizo kwa kujitegemea, na kushika njia ya kujiendeleza inayoendana na hali zao yenyewe. Pia amesisitiza kuwa China inaunga mkono kithabiti juhudi za nchi za kanda hiyo za kulinda mamlaka na ukamilifu wa ardhi.