Mashirika ya Umoja wa Mataifa yatoa wito wa msaada wa dharura kukabiliana na njaa nchini Uganda
2022-06-09 08:41:30| CRI

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yatoa wito wa msaada wa dharura kukabiliana na njaa nchini Uganda

 

Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Uganda yametoa wito wa msaada wa dharura wakati zaidi ya watu laki 5 wakikosa chakula katika mkoa wa Karamoja ulioko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Wito huo umetolewa baada ya ripoti ya Upambuzi wa Kina wa Awamu ya Usalama wa Chakula (IPC) kutolewa mjini Kampala, inayosema kuwa watu wanaoathirika wanakosa chakula karibu siku tatu kila mwezi. Pia ripoti hiyo inaonyesha kuwa idadi ya watu walioathirika imeongezeka na kufikia 518,000 mwaka huu, ikiwa ni zaidi ya watu 361,000 walioandikishwa mwaka jana.

Sababu kuu ya mgogoro huo imeelezwa kuwa ni vita inayoendelea nchini Ukraine iliyosababisha kupanda kwa bei za bidhaa ikiwemo chakula na mafuta.