Zaidi ya watu 40 wafariki katika poromoko la mgodi wa almasi nchini DRC
2022-06-10 10:35:34| CRI

Zaidi ya watu 40 wamefariki Jumanne jioni kutokana na kuangukiwa na kifusi katika mgodi wa almasi katikati mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Waziri wa mambo ya ndani wa serikali ya mkoa wa Kasai Alain Tshisungu Ntumba amethibitisha kuwa ajali hiyo ilitokea katika mji wa Samba, akisema maiti takribani sita tayari zimepatikana, na vikosi vya uokoaji bado vinaendelea kutafuta watu waliokwama kwenye kifusi.

Amesema watu waliofariki wote ni wachimbaji almasi wanaofanya kazi katika visima chini ya ardhi, na ajali hiyo imeathiri zaidi ya visima 40 vyenye kina cha mita 15 hadi 18.