Pembe ya Afrika kukabiliwa na hatari ya njaa
2022-06-10 09:27:15| cri


 

Mashirika ya Umoja wa Mataifa na wataalamu wa usalama wa chakula jana wametoa taarifa ya pamoja wakionya kuwa, uhaba wa mvua uliotokea kwa misimu minne mfululizo na majibu yasiyoridhisha ya ombi la msaada wa kibinadamu vinaweza kupelekea mamilioni ya watu nchini Ethiopia, Kenya, na Somalia kwenye ukingo wa njaa

Taarifa hiyo imesema, ukame mkali zaidi katika eneo la Pembe ya Afrika uliotokea tangu miaka minne iliyopita huenda hautapungua hivi karibuni, na inakadiriwa kuwa mvua kidogo zinaweza kunyesha kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba.