Shirikisho la wafanyabiashara wa China nchini Kenya latoa msaada wa vifaa kwa shule kwenye mtaa wa mabanda
2022-06-10 08:40:10| CRI

Shirikisho ya Uchumi na Biashara la Kenya na China (KCETA) jana limetoa msaada wa vifaa katika Shule ya Mcedo Beijing iliyoko kwenye mtaa wa mabanda wa Mathare jijini Nairobi, Kenya.

Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Liu Chenghui amesema, msaada huo unawakilisha ahadi ya Wachina wanaoishi nchini Kenya ya kutoa msaada wa kuboresha kiwango cha elimu nchini Kenya.

Mkurugenzi wa Shule ya Mcedo Beijing Benedict Kiage amesema msaada huo umefika katika wakati mwafaka kwani utasaidia kuboresha  hali ya kutoa mafunzo ya shule hiyo.

Msaada huo umejumuisha viti 87, kabati 70, meza sita, viti 35 vya chekechea, na madawati matano.