Nchi za Afrika zapata dozi milioni 818 za chanjo ya COVID-19
2022-06-10 08:40:59| cri

Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Maradhi  ya Afrika (Africa CDC) jana imesema, mpaka sasa nchi za Afrika zimepata dozi milioni 818 za chanjo ya COVID-19.

Kwa mujibu wa Kituo hicho, karibu asilimia 17.3 ya watu barani Afrika wamepata chanjo kamili ya COVID-19. Kufikia Jumatano jioni, idadi ya watu walioambukizwa virusi vya korona barani Afrika imefikia 11,675,825,  na vifo vya watu vilivyotokana na janga hilo vikifikia 253,518.