Hassan Sheikh Mohamud aapishwa kuwa rais mpya wa Somalia
2022-06-10 08:38:37| CRI

Hassan Sheikh Mohamud ameapishwa kuwa rais mpya wa Somalia katika hafla iliyofanyika chini ya ulinzi mkali mjini Mogadishu hapo jana, na kuhudhuriwa na viongozi kutoka Ethiopia, Misri, Djibouti na Kenya na wawakilishi kutoka nchi zaidi ya 20.

Katika hotuba yake, rais Mohamud ameahidi kuleta utulivu katika nchi hiyo inayokabiliwa na matishio na kuimarisha juhudi za kuleta amani na masikilizano nchini humo. Pia ameahidi kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi, kukabiliana na ukame mkali ulioikumba nchi hiyo, na kupunguza umasikini.

Ameiomba jamii ya kimataifa kuisaidia Somalia kukabilina na ukame mkali kuwahi kutokea nchini humo katika miaka 40 iliyopita, ambao katika miezi minne iliyopita, umewalazimisha zaidi ya watu laki 5 kukimbia makazi yao kutafuta maji na chakula.