UM: Misaada ya kibinadamu yaendelea kufika eneo la Tigray
2022-06-13 09:10:36| CRI

Ofisi ya uratibu mambo ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (UNOCHA) imesema hali ya jumla kaskazini mwa Ethiopia sasa ni tulivu japokuwa haitabiriki huku misaada ya kibinadamu inaendelea kufika katika eneo la Tigray.

Ripoti hiyo inasema tangu Aprili mosi hadi Juni sita, zaidi ya tani 65,500 za chakula zimepelekwa Mekelle, mji mkuu wa eneo la Tigray na kati ya hizo tani 14,700 zimesambazwa kwa watu zaidi ya 907,000. Misaada mingine itaendelea kusafirishwa kwa ndege kutoka Addis Ababa kwenda Mekelle.

Lakini imesisitiza kuwa sasa eneo la kaskazini Ethiopia bado linakabiliwa na vizuizi vingi vilivyotokana na ukosefu wa huduma za kimsingi na masoko yanayofanya kazi, uwezo dhaifu wa kupeleka vifaa, mafuta na fedha kwenye eneo hilo, changamoto za usambazaji kwenye maeneo yasiyofikika kirahisi, na uhaba wa washirika kwenye baadhi ya maeneo.

Takwimu za UNOCHA zinaonesha kuwa watu zaidi ya milioni 9 wanahitaji msaada wa chakula kaskazini mwa Ethiopia kwa mwaka huu.