China yatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutoa msaada wa kiujenzi kwa Mali
2022-06-14 08:34:29| CRI

Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutoa msaada wa kiujenzi kwa Mali.

Akiongea kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Mali, Balozi Zhang Jun amesema hali ya sasa nchini Mali ni ya kutatanisha, na jumuiya ya kimataifa inapaswa kuimarisha ufahamu wake wa kimkakati, kuainisha kazi zinazotekelezeka, kuweka vipaumbele na kutoa msaada wa kiujenzi wenye malengo.

Balozi Zhang amesisitiza kuwa China siku zote inawaunga mkono watu wa Afrika kutatua masuala ya Afrika kwa njia ya kiafrika, na kwamba mamlaka na uhuru wa kisiasa wa Mali ni lazima viheshimiwe.