Tanzania inapanga kuagiza boti 320 za uvuvi ili kuboresha sekta ya uvuvi
2022-06-14 08:31:02| CRI

Mamlaka nchini Tanzania zinapanga kuagiza boti mpya za kisasa 320 ndogo na za ukubwa wa kati ikiwa ni hatua ya kuleta mageuzi kwenye sekta ya uvuvi nchini Tanzania.

Waziri wa mifugo na uvuvi wa Tanzania Bw. Mashimba Ndaki ameliambia bunge mjini Dodoma kuwa uagizaji wa boti hizo ni sehemu ya mpango wa serikali kuleta mageuzi kwenye sekta ya uvuvi, na kuiwezesha sekta hiyo kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa.

Amesema boti hizo zitakazotumika kwenye uvuvi wa kina kirefu, zitaagizwa kwenye mwaka wa fedha 2022/2023.

Pia amesema serikali imeweka mikakati yenye lengo la kuwawezesha wavuvi kujenga viwanda vidogo vya kusindika samaki ili kuwawezesha kuongeza kipato chao.