Kenya yazindua maabara ya uchunguzi ili kuimarisha mapambano dhidi ya uhalifu wa kimtandao
2022-06-14 08:31:44| CRI

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amezindua maabara ya uchunguzi ya taifa ili kuimarisha mapambano dhidi ya uhalifu wa kimtandao, ambao umeendelea kuongezeka kutokana na maendeleo ya kasi ya uchumi wa kidigitali wa Kenya.

Rais Kenyatta amesema serikali itatumia mafunzo na ushiriki wa umma kwenye kupambana na changamoto mpya kama vile uhalifu wa kimtandao, ugaidi na magendo ya binadamu.

Maabara hiyo itakayogharimu dola za kimarekani milioni 34.98 pia itatumika kuharakisha uchunguzi wa uhalifu mkubwa kama vile mauaji, uporaji wa kutumia mabavu na ubakaji.

Rais Kenyatta pia amesema maabara hiyo itatumika kuchambua mafaili ya kidigitali yaliyopo na yaliyofutwa, na kurejesha barua pepe zilizofutwa na zilizosimbwa, video, anuani za mtandao wa internet na ujumbe mfupi wa simu.