Watu wasiopungua 50 wauawa katika shambulizi Burkina Faso
2022-06-14 09:23:58| CRI

Msemaji wa serikali ya Burkina Faso Bw. Lionel Bilgo amesema raia wasiopungua 50 wameuawa katika shambulizi lililofanywa na wapiganaji wasiojulikana usiku wa Jumamosi dhidi ya jamii ya Seytenga mkoani Seno, kaskazini mwa nchi hiyo. Amesema idadi ya vifo inaweza kuongezeka wakati kazi ya utafutaji bado inaendelea.  

Mbali na shambulizi hilo, mashambulizi mengine mawili yalitokea Alhamisi na Jumapili katika mkoa huo na kusababisha vifo na majeruhi wengi. Hali ya usalama nchini Burkina Faso imekuwa ikizorota tangu mwaka 2015, ambapo mashambulizi yamesababisha vifo zaidi ya 1,000 na watu zaidi ya milioni 1.9 kukimbia makazi yao.