Utafiti waonesha vijana wa Afrika wanaona China inatoa mchango chanya katika bara lao
2022-06-15 08:35:14| CRI

Ripoti iliyotolewa na Mfuko wa Ichikowitz wa Afrika Kusini inasema, vijana wa Afrika wanaona China ni nchi ya kigeni yenye ushawishi mkubwa zaidi katika bara lao, ambayo inatoa mchango chanya kwenye maendeleo ya miundombinu na mafunzo ya ufundi stadi.

Kura za Maoni za Vijana wa Afrika 2022, zilizofanyika katika nchi 19 za Afrika na kuchapishwa jumatatu, zinaonesha kuwa asilimia 76 ya vijana wanaona ushawishi wa China ni chanya, huku asilimia 77 ya wahojiwa wakiitaja China kuwa nchi ya kigeni yenye ushawishi mkubwa zaidi barani Afrika.