Uzalishaji wa chai Kenya waathiriwa na hali ya hewa isiyo ya kawaida
2022-06-15 08:52:31| CRI

Kurugenzi ya Chai ya Kenya imesema uzalishaji wa chai nchini Kenya katika robo ya kwanza ya mwaka huu umepungua kutokana na kuathiriwa na hali mbaya ya hewa, ikiwemo mvua isiyo ya kawaida, kiangazi cha muda mrefu na ukame.

Takwimu zinaonyesha kuwa uzalishaji wa chai nchini Kenya katika muda huo umepungua kwa zaidi ya kilo milioni 5 na kufika kilo milioni 135.83 ikilinganishwa na kilo milioni 140.98 za mwaka jana. Shirika hilo limeonya kuwa uzalishaji wa jumla nchini Kenya unaweza kuendelea kupungua wakati Kenya ikikabiliwa na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.